Top News

Mapinduzi Sudan : Waandamanaji wakaidi agizo la kutotoka nje baada ya Bashir kupinduliwa mamlakani

Waandamanji wanaoipinga serikali wameendelea kuingia mitaani kwa wingi katika mji wa Khartoum

Na Gad Oteba

Redio Mkarimu imebaini kuwa kuna hatari kubwa Sudan kwamba makundi tofauti ya usalama na wanamgambo wanawezachukua fursa hii ili kupigana na kuleta vifo.

Umati mkubwa umeendelea kuwepo katika mitaa ya mji mkuu wa Sudan , Khartoum, na kupuuza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku iliyotangazwa na baraza jipya la jeshi nchini humo.

Kiongozi wa muda mrefu wa Sudan Rais Omar al-Bashir alipinduliwa na kukamatwa siku ya Alhamisi baada ya miezi kadhaa ya maandamano nchini humo.

Jeshi mpya ilitangaza kuiongoza nchi hiyo kwa miaka miwili na kuitangaza miezi mitatu ya hatari.

Hii ni hatua ambayo imeibua hisia kali dhidi ya waandamanaji na kupingwa vikali wengi wao wakisema baraza la jeshi ni sehemu ya utawala uliong’olewa madarakani.

Hali hii mpya ya sitofahamu imeibua hofu kubwa ya uwezekano wa kutokea kwa makabiliano baina ya waandamanaji na jeshi.

Kulingina na wao wanashinikiza msimu mpya wa uongozi huku asilia kubwa wakitaka kuwepo kwa uchaguzi mpya nchini humo hivi karibuni.

Wanaandamanaji hao wamekiri kuendelea kuandamana mpaka watakapopata uhuru kamili.

Umoja wa Mataifa, Muungano wa Africa na Muungano wa ulaya wametoa wito wa kuwepo kwa hali ya utulivu Sudan.

Moussa Faki mwenyekiti wa Muungano wa Africa Jana alisema mapindizi si njia thabiti ya kutatua shida zilizoko nchini humo.

Aidha ameomba kuwepo na utulivu wakati wanaendelea kujadiliana na halmashauri ya amani na marithiano Africa  wakitafuta suluhu ifaayo kwa nchi hiyo.

Bashir anakabiliwa na kibali cha kukamatwa kilichotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), ambayo inamshutumu kwa kupanga uhalifu wa kiviuta na uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × = 7